Luke 24:34-39

34 awakisema, “Ni kweli! Bwana amefufuka, naye amemtokea Simoni.” 35 bKisha wale wanafunzi wawili wakaeleza yaliyotukia njiani na jinsi walivyomtambua Isa alipoumega mkate.

Isa Awatokea Wanafunzi Wake

(Mathayo 28:16-20; Marko 16:14-18; Yohana 20:19-23; Matendo 1:6-8)

36 cWalipokuwa bado wanazungumza hayo, Isa mwenyewe akasimama katikati yao, akasema, “Amani iwe nanyi!”

37 dWakashtuka na kuogopa wakidhani kwamba wameona mzuka. 38Lakini Isa akawauliza, “Kwa nini mnaogopa? Kwa nini mna shaka mioyoni mwenu? 39 eTazameni mikono yangu na miguu yangu, mwone kuwa ni mimi hasa. Niguseni mwone; kwa maana mzuka hauna nyama na mifupa, kama mnionavyo kuwa navyo.”

Copyright information for SwhKC